Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro
alisema “Kukweli ni nimekwazika sana pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba.
Baada ya muda ya nikamtafuta tena vipi ili tufanye kabisa ile
nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri lakini.Lakini nashangaa
sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo ameeimba yeye tena alafu kibaya
zaidi ametumia beat ile ile pia na mashairi yale yale.
Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri,kwani watu wote
tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake.Na usiku wa
jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya.
No comments:
Post a Comment