Monday, July 29, 2013

NENO LA FRANK MWAKALEBELA KUHUSU SOKA LA TANZANIA

AMA kweli soka lina maajabu na kila mdau au shabiki wa mchezo huu atakubaliana nami katika hili kwani inaeleweka kabisa. Lakini maajabu ya soka la Tanzania ni tofauti na sehemu zote duniani. 
http://api.ning.com/files/rgZ912HEgGz934ooTqi-cGZ*HCNQmgTJbfhRQ78rez1t-ACjL0I0g0YTkU6G4dWxIAusIo*iTqjgN9bdOkE*0l7pL36lR5sF/mwakalebela.jpg?width=239
Soka la Tanzania lina maajabu ndani na nje ya uwanja ingawa kwa maajabu ya ndani ya uwanja, hatuwezi kuwashinda ndugu zetu wa Nigeria walioweza kufungana hadi mabao 69-0 ndani ya dakika 90! 

Nje ya uwanja ndiko kuna maajabu yake hapa Bong, Kwanza mfumo wa uendeshaji wa klabu zetu ni tofauti sana na kwa wenzetu, lakini kubwa ni pale baadhi ya viongozi wanapoamua kuzifanya klabu kama mali binafsi. 

Inawezekanaje mtu akajimilikisha, japo kwa muda, klabu kubwa kama Simba au Yanga? Inawezekanaje mtu akajiamulia anavyotaka huku wanaojiita ‘wanachama’ wakipiga makofi? 

Wanachama vigeugeu wa aina ya wale tuliowashuhudia Jumamosi kule Police Officers Mess Oysterbay, hawatufai na ni hatari kwa ‘maendeleo endelevu’ ya klabu na soka kwa ujumla.

WANANDOA WALIOZALIWA SIKU MOJA, WAFA SIKU MOJA

Wanandoa katika Jiji la California waliozaliwa siku moja na kuoana siku moja miaka 75 iliyopita wamefariki  dunia siku moja.
Couple Born on Same Day, Married 75 Years, Die One Day Apart
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA FIRAUNI…
 


Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Long Beach Press Telegram, Helen na Les Brown walifariki Julai 16 na 17 mwaka huu wote wakiwa na umri wa miaka 94.

Zach Henderson, Mmilikii wa Grosari moja ijulikanayo kwa jina la Ma N’Pa iliyopo Long Beach alinukuriwa wakisema kuwa alikuwa akiwaona wapendanao hao kila siku iitwayo kwa Mungu na kuuita uhusiano wao kuwa “ a Wonderful Blessing”.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Press –Telegram imesema kuwa wote walizaliwa siku moja yaani Desemba 31, 1918 na pia walianza kuwa pamoja mwaka 1937 katika masomo ya sekondari.

Imejulikana kwamba wanandoa hao walikuwa waamini wa Mashahidi wa Yehova (Jehova Witnesses) waliobarikiwa kuwa na mtoto wao Les Brown Jr.

Henderson anasema imani yao kwa Mwenyezi Mungu ndio iliyozidi kuimarisha ndoa yao hadi kufikia hapo.

Mtoto wao Les Brown Jr alinukuriwa akisema “Walikuwa pamoja kila siku kwa miaka 75, hakika upenndo wao ulilandana” 

Post Telegram limeripoti kuwa Les Brown alikuwa akiumwa ugonjwa wa Parkison’s na mkewe Helen Brown alikuwa akisumbuliwa Kansa ya tumbo hadi mauti yao yalipowakuta

"She was completely cognitive," Henderson said, describing how he found Helen Brown a few days before she died. "It seems like she was waiting for Les to be comfortable and they were going to move on to something else with each other."

Ibada ya pamoja itafanyika siku ya Jumamosi mchana kwa ajili ya kuwakumbuka wanandoa hao huko Long Beach, California.

CHANZO: ABC NEWS/YAHOO NEWS