Sunday, April 7, 2013

TUSIMSAHAU STEVEN KANUMBA (THE GREAT KANUMBA): Zitazame picha zake mbalimbali wakati wa uhai wake.


Habari za msiba wake zilianza kuenea na kusambaa kama moto wa nyika usiku wa Ijumaa tarehe 7 mwaka 2012.Kila aliyepata taarifa hakuamini. Ilikuwa ni kama ndoto au jinamizi tu ambalo baada ya muda litapita na kila kitu kitakuwa sawa.
Kulipokucha,taarifa ambazo zilianza kama uvumi na kutoaminiwa na wengi, zikaanza kuthibitishwa na watu mbalimbali hususani waliokuwa naye karibu usiku ule.Uvumi ukawa ukweli. Steven Charles Kanumba akawa ameiaga dunia tarehe 7 April, 2012 akiwa na umri mdogo tu wa miaka 28 (Steven alizaliwa tarehe 8 Januari mwaka 1984 mkoani Shinyanga) .Kifo chake kikaacha huzuni na majonzi makubwa hususani kwa mashabiki wake na wa filamu ndani na nje ya Tanzania wakiwa hawaamini na kulia kwa uchungu usio kifani.



THE LATE STEVEN KANUMBA (1984-2012)
Kilichofanya taarifa za kufikwa na mauti kwa Steven Kanumba kuwa ngumu kuingia akilini mwa watu zinatokana na ukweli kwamba wengi walikuwa wamemuona jana yake na wengi walikuwa wamewasiliana naye. Kanumba alikuwa mtu wa watu. Aliongea na kila mtu na bila shaka ndio maana alipendwa na wengi. Aliwathamini mashabiki wake na hata wale ambao hawakuwa mashabiki wake. Iweje uniambia Kanumba amefariki? Nini kimetokea?Wengi walihoji kwa masikitiko.
Taratibu nchi nzima ikaanza kupata taarifa na uthibitisho. Vyombo vya habari hususani redio zikaanza kuwasaidia wananchi kuomboleza. Nyimbo za maombolezo zikatawala na huku takribani kila redio ikibadili ratiba ya vipindi vyake ili kwenda sambamba na tukio zito lililokuwa limetokea; msiba wa msanii mahiri wa filamu, Steven Charles Kanumba.

Siku tatu baadae, mazishi ya Steven Kanumba yalifanyika.Umati mkubwa wa watu ambao haukurajiwa na yeyote ikiwemo kamati ya mazishi yake, ukajitokeza kumuaga mpendwa wao. Viwanja vya Leaders pale Kinondoni vikarindima na vilio. Watu wakazimia na wengine wengi kushindwa kujua wafanyeje. Ni picha ambayo mpaka leo hii haijatoka vichwani mwa watu waliohudhuria.

Leo hii, mwaka mmoja baadae, tunamkumbuka Steven Charles Kanumba. Yeye alithubutu pale ambapo wengi walidhani hapawezekani. Alijaribu kwa nguvu na akili zake zote kuitoa sanaa ya filamu katika mipaka ya Tanzania.Alifanikiwa. Alipofariki salamu za rambirambi zilitoka kila kona ya Afrika. Waghana walimlilia.Wanigeria walibubujikwa na machozi…Wakenya walilia…kila kona ya bara la Afrika walimlilia.

Kanumba alikuwa msikivu na mwepesi wa kujifunza. Maringo aliyokuwa nayo ni ya kibinadamu. Ni yale ya kujikubali mwenyewe kwanza ili wengine nao waanze kukukubali. Alitambua wazi umuhimu wa mashabiki na watizamaji wa filamu. Alithamini mchango wao kwa vitendo. Yeye ni miongoni mwa wasanii waliojitolea sana katika shughuli za kijamii. Alichangia na kuhamasisha.

Mwaka mmoja baadae; tunamuezi vipi? 

***Endelea kupumzika kwa amani Steven 

Kanumba.***


                 

PICHA MBALIMBALI ZA KANUMBA ENZI ZA UHAI

 WAKE




Akiwa amepokea tuzo muigizaji bora Tanzania

Steven Kanumba na Swaiba wake Ray.

Steven Kanumba

Kanumba

Ni Katika moja ya filamu yake

Katika filamu yake inayoitwa "THE CRAZY LOVE" Humo alikua na Hemedi, Shamsa Ford Na wengine kibao.

Akiwa pamoja na mshiriki wa Big Brother Africa (BBA) Mr. Richard

Ni katika Magic House

Enzi zake Kaole sanaa Group

Cover-photo ya movie yake ya "ANCLE JJ"

Akiwa na moja ya Mwanadada aliyemlta kwenye industry ya film Tanzania

Akiwa ametokelezea

Kaburi lake lililopo Kinondoni-Tanzania



Moja ya picha akiwa ndani ya film yake ya "YOUNG BILLIONAIRE"

Ni katika Film ya "THE SHOCK"

Akiwa Irine Uwoya

Akiwa katika scene ya "BIG DADY"

Kanumba & Lady Jay Dee

Akiwa na Maswaiba wake

Akiwa na Marafiki zake

Ndani ya the Mboni Talk Show

Katika film ya "FAKE SMILE"

Ni katika movie ya  "DEVIL KINGDOM" Alimleta msanii maarufu wa Nigeria Ramsey Noah (wa tatu kutoka kushoto).

Kanumba


Kanumba & Aunt Ezekiel

Kanumba & Jaquline Wolper

Ni katika harakati za kuuaga mwili wake Katika Makaburi ya Kinondoni
Kanumba (The Great)

Mama Mzazi wa Kanumba
Ni katika Maandalizi ya Film Yake ya "THE BIG DADY" Iyotoka Mwaka 2012








No comments:

Post a Comment