Saturday, March 23, 2013

WIZARA YA ELIMU YAKANA KUWATAPELI WALIMU


WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekana kuhusika kwa namna yoyote kuandika barua ya kuwaita walimu kwenye semina hewa iliyokuwa ifanyike mkoani Morogoro kuanzi Machi 11 hadi 26 mwaka huu.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYmClo80XRGW2w0L2mdVWGrAlYDYWbLXdasTYKpBwW16g_AqAx7_loqEwDmi4UjL5WfMDfpjGhDjYrncmyygj39r39j3hM849hX9NQcwIJECllePfrW7ssAmwyqxVeJZxsEyOO3hPzqeJU/s1600/Dk+Kawambwa.JPG
Hatua hiyo inakuja baada ya gazeti hili kuchapisha habari kuhusu baadhi walimu kudai kutapeliwa kwa kutumiwa nakala ya mwaliko na hivyo kuingia hasara ya gharama za usafiri na malazi.

Nakala ya barua hiyo yenye Kumb. Na. AHRD /98/789/03S//40 ya Februari 18, 2013 ilisainiwa na mtu aliyejitambukisha kuwa ni O. L. Michael kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara hiyo ikiwataka kuhudhuria semina ya kitaifa ya rushwa, ukimwi, uzalendo na uwajibikaji kwa walimu wa Tanzania Bara.

Walimu hao walidai kuwa mbali na barua hiyo, pia walipigiwa simu kupitia namba 0756 018031 kwa msisitizo ikiwaomba kuhudhuria pasipo kukosa.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu kufafanua suala hilo, Ofisa habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alitoa sababu tano kuonesha uongo huo uliofanywa na watu wasiojulikana.

Alisema kuwa wizara inapoandika barua kwa mwalimu haiendi moja kwa moja kwake bali kupitia mwajiri wake ambaye ni halmashauri.

Bunyazu aliongeza kuwa hata jina la mwandishi wa barua hiyo O. L. Michael si mtumishi wa wizara na kumbukumbu namba iliyotajwa haipo wizarani.

“Hata Chuo cha Ualimu kilichotajwa cha Kigurunyembe hakiitwi hivyo bali kinajulikana kama Chuo cha Ualimu Morogoro. Halafu barua ingetoka wizarani, Kamishna wa Elimu asingeweza kupewa nakala,” alifafanua.

Barua hiyo ilisema kuwa wizara kwa ushirikiano na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zingefanya semina ya kitaifa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwa pamoja kuanzia Machi 11 hadi 26 mwaka huu, katika Chuo cha Ualimu cha Kigurunyembe kilichopo mkoani Morogoro.

Ikiwa na muhuri wa wizara, barua hiyo ilionesha kuwa nakala zake zilitumwa pia kwa Kamishna wa Elimu, Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU na Mkurugenzi wa USAID na kuambatanishwa na ratiba.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

Friday, March 22, 2013

MWANDISHI MKUBWA WA AFRIKA (CHINUA ACHEBE) KAIAGA DUNIA


Mwandishi mashuhuri wa vitabu nchini Nigeria Chinua Achebe, ambae alikuwa anatajwa kuwa ndie babu wa fasihi ya kisasa barani Afrika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

 http://achebebooks.com/wp-content/uploads/2011/11/Chinua-Achebe-speakn-abt-thingsfallapart1.jpg
Msemaji wa kampuni ya Penguin ya mjini London inayochapisha vitabu vya Achebe alitangaza kifo chake kupitia barua pepe aliyoituma katika  mashirika ya habari. Vyombo vya habari nchini Nigeria viliripoti kuwa Achebe alifariki katika hospitali mjini Boston, Massachusetts Marekani. Achebe alifahamika zaidi kutokana na kitabu chake cha hadithi cha 'Things Fall Apart' cha mwaka 1958, ambamo alizungumzia kisa cha msuguano baina ya watawala wa kikoloni wa Uingereza na utamaduni wa watu wa kabila la Igbo, katika eneo alikozaliwa kusini-mashariki mwa Nigeria.

ESTHER BUKUKU NA MUZIKI WA INJILI


“Tasnia ya Uimbaji hususani wa nyimbo za Injili hapa nchini kuna wakati unakwaza kweli na kwa upande mwingine unabariki” …


Ndivyo alivyoanza kujieleza Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Esta Bukuku katika mahojiano na JAIZMELALEO (Mtangazaji wa Radio Kili Fm Na mmiiki wa blog ya http://jaizmelaleo.blogspot.com/) siku chache zilizopita.

Esther Bukuku ambaye ni muumini wa Madhehebu ya Kipentekoste ni mama wa watoto watatu ambao ni Eli, Kelvin na Benjamin anafanya kazi zake nchini za kupeleka ujumbe wa Neno la Mungu kwa njia ya Uimbaji uliotukuka.

Hadi hivi sasa ana Albamu moja tu aliyoitoa mwaka 2011 “WATESI WANGU” 

Alipoulizwa ni kwanini aliipa jina hilo Mwanamke huyo mwenye Mume mmoja anayeitwa Jojo Sanga  alisema kuna wakati alaipitia mapitoa amabayo ahakuyataja isipokuwa alisema mambo amabayo yalimsononesha sana hata kufikia wakati ambao alihisi kuna watu wanafurahi jinsi anayopitia masahibu hayo.

CHANGAMOTO
ESTHER (Esta) Bukuku anasema katika Muziki wa Injili una changamoto zake kwa sasa kutokana na ukweli kwamba kuna waimbaji wengine wamekaa kibiashara zaidi hali ambayo imeshusha sana kiwango cha kazi zao.

Pia anasema jamii imekuwa ikiwaibia haki miliki. Hapa aligusia mkataba ambayo anaingia na msambazaji wa kazi ya muziki kwamba wamekuwa wakiwaibia kutokana na kuendelea kutoa “copy” zaidi bila ya faida kwa mwimbaji ambaye ndiye aliyetakiwa kufaidika.

WITO
Esta Bukuku ametoa wito kwa jamii kuacha “ku-burn” kazi zao kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
ESTHER BUKUKU AKIWA NA MCHUNGAJI BUKUKU KANISANI

ESTHER BUKUKU hufanya ibada zake katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Amani Cathedral Centre Soweto Moshi kwa Mchungaji Benjamin Bukuku.