Tuesday, August 6, 2013

Chimwemwe atamba kumchapa Cheka

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo Makame (katikati) akiwatambulisha mabondia wawili kutoka Malawi,  Chiotcha Chimwemwe (kushoto) na Bgright Mdoka (kulia) kwa waandishi wa habari tayari kwa mapambano yao ya Agosti 10. Cimwemwe  atapambana na Cheka wakati Mdoka atazipiga na Jitu Samia. Mwingine katika picha ni promota wa Chimwemwe, Steven Msiska.


BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa wa Malawi, Chimwemwe Chiotcha amewasili nchini na kutamba atamtwanga bondia alisyekuwa na mpinzani Tanzania, Francis “SMG” Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Chimwemwe ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi zaidi ya kupigwa kwa pointi na Cheka Desemba 27 mwaka jana, alisema kuwa amekuja kulipiza kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa sana.
Alisema kuwa hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO) utokea ulingoni tu na wala si ushindi wa kupangilia. “Nimekuja hapa kushinda na wala si vinginevyo, nakuja Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na matokeo ya awali na ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua nitaibuka na ushindi,” alisema Chimwemwe.
Alifafanua kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na Cheka na kushindwa kuwa hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa mabondia hao. Mimi nimedhamilia kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni fursa yangu,” alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa pambano hilo, Zumo Makame alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika na siku hiyo kutakuwa na mapambano makali nay a kusisimua.
Makame aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania ubingwa wa Taifa wa Shirikisho la Masumbwi la PST dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid “Snake Man” Matumla atazichana na Maneno “Mtambo wa gongo “ Oswald na bondia mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
Mapambano mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude atapigana na Juma Kihiyo katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson (featherweight) na  Karim Mandonga dhidi ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter.
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'TitoTrinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchini.

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA MUHEZA TANGA SIKU YA IDI PILI

MPAMBANO  mwingine wa masumbwi unatarajia kufanyika Muheza mkoa wa Tanga wakati wa siku kuu ya idi pili kwa ajili  ya kutoa burudani kwa wakazi wa Muheza akizungumza kuhusu mpambano huo mratibu wake ambaye ndiye mwandaaji wa mpambano huo Hatibu Mwijuma amesema mpambano huo umeandaliwa maalumu kwa ajili ya kutoa burudani wakati wa sikukuu ya Idi na mpambano utafanyika katika viwanja vya jitegemee



Mpambano huo utakaowausisha mabondia kutoka Dar es salaam na wa Muheza, Mbena Rajabu wa Dar atakaeoneshana kazi na Jumanne Mohamedi mpambano wa raundi sita huku George Allan wa Muheza ataoneshana ubabe na  Muhamed Meme wa Tanga

Mapambano mengine mengi ya kukata na shoka uku kukiwa na burudani ya muziki alitaja kiingilio kwa siku hiyo kwa kuwa tunaitaji kila mtu aje kushudia mchezo wa ngumi kwani  ni nafasi ya pekee tuliyoipata kingilio kitakuwa ni 2000,kwa 1000,


Ili watu waweze kuangalia ulinzi ni wa uwakika mchezo uho utakaosimamiwa na Oganaizeshani ya ngumi za Kulipwa nchini TPBO umereta faraja kwa wakazi wa muheza kwani wana kiu kubwa ya kuangalia mchezo huo wa masumbwi unaopenda na watu wengi

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AFUTARISHA IKULU JANA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akiwa na Viongozi wakati wa futari aliyowaalika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo usiku.
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(wa pili kulia) akiwa na Viongozi akina mama wakati wa Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo usiku.
 Baadhi ya Akina Mama walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,leo usiku katika viwanuja vya Ikulu Mjini Zanzibar.
  Wananchi mbali mbali wa Manispaa ya Mji wa Unguja,waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaaafu wa Zanzibar alhaj Dk.Amani Abeid Karume, baada ya futari aliyowaalika wananchi katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na wananchi katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku,baada ya futari aliyowaalika katika mwezi huu wa Ramadhan. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.