Saturday, September 7, 2013

FAHAMU WASIFU WA ELIZABETH MICHAEL (LULU) HAPA


Elizabeth Michael
Lulu mwigizaji Bora wa kike wa filamu 2013/14 ZIFF.
Mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael ‘LULU’ kama lilivyo jina lake kwa sasa ni lulu kweli katika tasnia ya filamu, inaaminika kuwa binti huyo ambaye ni hivi karibuni tu ndio alikamilisha umri wa kuwa mtu mzima baada ya kuwa chini ya miaka 18 naye kuingia katika kundi la wasanii wa kike na kuteka kundi hilo.
.
Elizabeth Michael
Lulu akiwa katika pozi la kucheza muziki na kuimba katika uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age.

Lulu ambaye ndiye mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2012/2013 kupitia tuzo zilizotolewa na Zanzibar International Film Festival, anasema kuwa amekuwa na kuwa Lulu mpya mwenye majukumu ya kuelimisha jamii, baada ya kutolewa gerezani kwa dhamana Lulu jambo la kwanza ambalo amelifanya ni kuzindua filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish age.
Filamu ya Foolish age ilizinduliwa Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa filamu, Lulu aliweza kuongea na kuipongeza kampuni inayomsimamia ya Proin Promotion kwa kumpa nafasi ya kuwafunza wengine kwa mambo aliyopitia huku akiwa kama mtoto ambaye hakupenda sana kuwasikiliza wakubwa zake.
Nilitumia fursa hiyo kutaka yeye ni nani aliingiaje katika tasnia ya filamu na kuwa gumzo la filamu anasema kuwa yeye alianza kuigiza akiwa na miaka minne, lakini hakuwa maarufu, lakini akiwa na umri wa miaka saba alikutana na Mahsein Awadh ‘Dr. Cheni’ katika bonaza ambalo pia Dr. Cheni aliaandaa Talent Show, Elizabeth Michael akiwa na mama yake alimweleza Dr. Cheni kama anaweza kuigiza.
“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Bonaza pale Dar west Park ndipo nilipokutana Elizabeth akiwa na mama yake lakini alionyesha maajabu pamoja na udogo aliokuwa nao, katika Talent show yeye aliibuka namba moja huku akiwa amewatupa wasanii wengine mbali hadi Masanja Mkandamizaji alipitwa na Lulu naye akaangukia mshindi wa tatu kwa wakati ule,”anasema Dr. Cheni.
.
Mahsein Awadh
Dr. Cheni akiongea kwa hisia kuhusu msanii wa kike Lulu katika mahojiano.

Dr. Cheni anasema kuwa yeye alimchukua hadi Magomeni na kumkabidhi katika uongoza wa kundi la Kaole Sanaa Group, Lulu alifanyiwa usaili na kupitia kwa asilimiakubwa na kupendwa na kila msanii, lakini jukumu kuu kuhusu usalama na kila jambo lilikuwa kwa Dr. Cheni ambaye baadaye kufuatia mabadiliko ya Lulu kwake Dr. Cheni ilikuwa tatizo kwani kila kitu kibaya kilichofanywa na Lulu lawama ilikuwa kwake kutoka kwa mama yake.
Baada Lulu kuwa mwanakundi la Kaole alichagua jina lake la Nemu na kukubalika na kundi la Kaole na kuanza kuigiza akiwa na kundi hilo na alikuwa ni kipenzi cha waigizaji wote kwani moja ya sifa yake ilikuwa ni usafi na kujipenda toka akiwa mdogo , jambo ambalo hata Herieth Samson ‘Kemmy’ alishikwa na mshangao baada kufungua handbag ya lulu.
.
Herieth Samson kakulu
Kemmy mtu aliyemlea Lulu kisanaa

Mshangao aliopata Kemmy ni pale alipoona vitu ambavyo mara nyingi utakiwa kuwanavyo akina dada lakini Lulu alikuwa na vitu vya kujiremba na kama mtu mzima na hata pale alivyomuuliza vitu vile ni vya nani ? Lulu alimjibu kwa kujiamini tu bila hofu kama ni vitu vyake kwa ajili ya matumizi yake kama mwanamke Kemmy alizidi kushangaa.
“Siku hiyo nilichukua mkoba wa Lulu na kukuta kuna lipstick, poda, leso nyeupe, wanja na kioo, pamoja na funguo wa mlango nikamuuliza vitu hivyo ni vya nani akasema kuwa vyangu mama bwana si unajua kuwa mimi ni msichana kumbuka alikuwa na miaka saba tu, kwa hiyo hayo yalikuwa maisha ya Lulu mtu wa kujipenda,”anasema Kemmy.
Kemmy anasema kuwa baadaye Lulu alizidi kubadilika na kupenda mavazi mafupi ndipo alipomtafauta na kumuomba aongee naye lakini siku hiyo yenyewe alikuwa kava nguo fupi sanaa maana aliamua kumtafuta baada ya kuona picha mbaya katika moja ya gazeti hata hivyo aliongea naye lakini maongezi yale hayakuzaa matunda pale alipopata matatizo na kwenda jela.
Lakini Kemmy anasema Lulu kakua ameonyesha uwepo wa Mungu kwake, Lakini unajua jina la Lulu aliyelitunga na kuwa maarufu? Jina hilo lilitungwa na Salum Mchoma ‘Chiki’ mtunzi wa mchezo wa Tetemo ndiyo alimbadilisha kutoka jina lake la Nemu na kumwita Lulu na leo kweli jina linamaananisha ndoto za Chiki.
“Ndoto zangu zimeonekana wakati ninaandika mchezo wa Tetemo nikampa jina la Dhahabu lakini kwa sababu tulikuwa na uhusiano na Mr. Chuzi akaniomba nibadilishe jina la Dhahabu ili tusiwachanganye watu maana naye alikuwa na Jumba la Dhahabu, ndipo nikampa jina la Lulu hadi leo kawa msanii nyota na Lulu kweli ndoto zangu zimetimia,”anasema Chiki.
Lulu anasema amepitia mengi katika maisha yake hata mama yake anajua mateso aliyompa mambo ambayo hataki kuyarudi kwani kufuatia mkasa ulimpata ilikuwa ni njia moja ya yeye kupata fursa ya kuifundisha jamii kupitia sanaa hiyo na ndiyo maana ameandaa filamu inayoelezea maisha yake akiwa chini ya miaka 18, anatumia kuwaambia vijana wanavyokuwa katika umri huo wasipuuze ushauri kutoka kwa wakubwa zao.
.
Salum Mchoma
Chiki Mchoma aliyempa jina la Lulu.

Elizabeth Michael, mama yake.
Lulu akifurahia na mama yake mzazi katika muziki

Elizabeth Michael.
Lulu akiwa na mama katika pozi.

“Sikumsikiliza mama yangu wakubwa zangu, nilikuwa kizani yale niliyoyafanya ndio niliamini kuwa sahihi, sikuona hatari mbele yangu lakini nahisi ulikuwa mpango wa Mungu kwa tukio lilonitokea, watu walinihukumu lakini ukweli wa hili ni Mungu pekee anayejua ukweli, kwa sasa nampenda Yesu ninaomba na kusali Lulu amekua Lulu ni mpya ninataka kuelimisha jamii kwa kupitia maisha yangu,”anasema Lulu.
Akiongea zaidi alisema kuwa hawezi kuongelea sana mambo yalimtokea kuhusu marehemu Kanumba kwa sababu kesi hiyo bado ipo mahakamani, amepania kufanya kazi kwa nguvu lakini kupitia matatizo yake kajifunza mengi na hataki kurudi huko na anashukru kupata kampuni ya Proin Promotion ambayo ndio wanaomsimamia hawezi kushiriki filamu yoyote kutoka nje ya kampuni hiyo.
.
Elizabeth Michael.
Lulu katika gauni kali na la kuvutia katika pozi.

“Lulu alinitesa hadi nilikuwa napata shida na kuhahaa, lakini nimejifunza kwake kwani mwanangu kabadilika na kuwa mtu mzima anayejua nini anafanya kumbe ilikuwa utoto tu, lakini nimejifunza kutoka kwake mimi nilikuwa mkali sana hiyo ilichangia Lulu kuniogopa na kuwa mbali na mimi pale anapokosa, wazazi tuongee na watoto wetu kwa upole,”anena mama yake.
Lulu ndiyo mlezi wa familia yake mama anafaidika na mtoto wake huku Lulu akimsomesha mdogo wake shule ya kimataifa kwa kumlipia ada na gharama zote, mwenye anasema yupo katika taratibu za kuendelea na shule kwani moja ya malengo yake kuwa mwigizaji wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kupitia filamu anaamini anaweza kufanya hilo Mungu amsaidie.
Baada ya filamu ya Foolish age Lulu anatarajia kutoa filamu ya Mapenzi ya Mungu kazi ambayo amemshirikisha mama yake marehemu Kanumba Frola Mtegoa filamu ambayo nayo bado itakuwa ikiongelea sana maisha na mikasa ya maisha na Lulu ameahidi kutotengeneza wala kuigiza filamu za mapenzi ambazo zimeshamiri Bongo, michezo iliyomtoa Lulu ni, Tetemo, Jahazi, Dira, Tufani,
Gharika na Baragumu.

No comments:

Post a Comment