Saturday, September 7, 2013

MATESO MAKALI YAMPELEKEA AGNES MASOGANGE NA MELLISA KUWATAJA WALIOWATUMA UNGA

http://1.bp.blogspot.com/-E8D0JNv7MGo/Uigre_VSWkI/AAAAAAAAlTk/aCD6AiD9Alg/s1600/agness.jpgAgnes Gerald ‘Masogange’ na shosti wake, Mellisa Edward kabla ya kupandishwa kizimbani kwa msala wa dawa za kulevya ‘unga’ Afrika Kusini waliingizwa kwenye chumba cha mateso kwa saa 24 ili kutaja waliowatuma.

Habari kutoka kwa chanzo chetu kilichopo jijini Johannesburg nchini humo zilidai kuwa baada ya kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, walipelekwa polisi ambapo walichukuliwa maelezo.

Ilielezwa kuwa mwanzoni waligoma kueleza mzigo huo wa kilo 150 wa unga ulikuwa wa nani hivyo ikabidi polisi wa upelelezi watafute njia nyingine ya kuwalainisha kwa kuwabembeleza kuwa wakieleza ukweli wataachiwa.

Chanzo hicho kilisema kuwa baada ya mbinu hiyo kushindikana ndipo wawili hao wakaingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ikiaminika kuwa watasema aliyewatuma.

“Unajua Sauzi (Afrika Kusini) huwa hawana utani na ishu za madawa ya kulevya. Jamaa (polisi) wana kila aina ya mbinu ya kumfanya mtu aeleze ukweli.

“Katika kutesa unaweza kuingizwa kwenye chumba maalum cha mateso ambayo nayo huwa yana steji zake.

“Kwanza utaanzia kwenye chumba kilichojazwa siafu wakubwa na huko unaweza usijue kuwa kuna siafu zaidi ya kuona kitu kama red carpet (zuria jekundu) kuanzia sakafuni, ukutani hadi kwenye dari, kumbe wale wote ni siafu.

“Wakishakuingiza mle ndipo utashangaa wale siafu wanacharuka na kuanza kukung’ata mwili mzima, zoezi hilo hufanyika kwa saa 24. Lazima useme ukweli.

“Kama bado ukijifanya mbishi au nunda ndipo unapelekwa hatua nyingine ya kulazimishwa kujisaidia haja ndogo kwenye waya wa umeme.

“Si unajua tena waya wenye umeme na maji vikikutana nini kinatokea? Lazima itatokea shoti ya kutisha kwani ule waya hufuata sehemu yale maji yanapotokea.

“Kinachofuata ni mtu kupigwa shoti kali ya umeme ambapo lazima utasema tu.

“Hicho ndicho kilichowapata akina Masogange kama wanavyofanyiwa Wabongo wengine wanaokamatwa Mitaa ya Rissik hapa Johannesburg.

“Baada ya mateso hayo, waliwataja waliowatuma mzigo huo wa unga aina ya crystal methamphetamine wenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8,” kilisema chanzo hicho ambacho ni Mbongo ambaye kwa sasa ni mkazi wa Mtaa wa Rissik, Johannesburg, wanapoishi Wabongo kwa kuungaunga aliyewahi kukumbwa na mkasa kama huo.

Habari za ndani zilidai kuwa baada ya kupitia mateso hayo, mabinti hao waliwataja watu wawili waliowatuma kusafirisha mzigo huo, mmoja akiwa ni mtoto wa kigogo ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania (jina lipo).

Ilidaiwa kuwa mtoto huyo wa mkubwa ni mjanja wa mjini ambaye alihusika kushughulikia kusafirisha mwili wa msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyefia Johannesburg Juni, mwaka huu.

Ilivuja kuwa mwingine aliyetajwa na akina Masogange ni mfanyabiashara maarufu Bongo anayesafiri nje mara kwa mara huku jina la ‘mtoto wa mjini’ Mangunga likitajwa zaidi hata na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison George Mwakyembe.

Kamanda wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, alikiri kupewa majina hayo lakini akaliomba gazeti hili kutoyachapisha kwa sasa kuepuka kuvuruga ushahidi.

Baada ya polisi wa upelelezi na wale wa kimataifa (Interpol) kujiridhisha na maelezo ya mabinti hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya pili Agosti 19, mwaka huu chini ya ulinzi mkali kama ule ‘anaowekewaga’ Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda anapofikishwa kwenye mahakama mbalimbali nchini kwa kesi zake za madai ya uchochezi.

Habari kutoka Sauzi zilieleza kuwa akina Masogange walipandishwa tena kizimbani hivi karibuni ambapo tayari kesi yao imeanza kuunguruma ikielezwa kuwa endapo watakutwa na hatia watakula mvua ya kifungo si chini ya miaka 10 kwa sheria za nchi hiyo.

Masogange na Mellisa walinaswa nchini humo Julai 5, mwaka huu wakiwa na mabegi sita yaliyokuwa na mzigo huo wa unga.

PICHA ZA SERENGETI FIESTA MKOA WA MBEYA

Fiesta mbeya 6
Fiesta Mbeya 7
Fiesta mbeya 8
Fiesta Mbeya 4
fiesta Mbeya 5
fiesta mbeya 3
Fiesta Mbeya 2
2
1
4

FAHAMU WASIFU WA ELIZABETH MICHAEL (LULU) HAPA


Elizabeth Michael
Lulu mwigizaji Bora wa kike wa filamu 2013/14 ZIFF.
Mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael ‘LULU’ kama lilivyo jina lake kwa sasa ni lulu kweli katika tasnia ya filamu, inaaminika kuwa binti huyo ambaye ni hivi karibuni tu ndio alikamilisha umri wa kuwa mtu mzima baada ya kuwa chini ya miaka 18 naye kuingia katika kundi la wasanii wa kike na kuteka kundi hilo.
.
Elizabeth Michael
Lulu akiwa katika pozi la kucheza muziki na kuimba katika uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age.

Lulu ambaye ndiye mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2012/2013 kupitia tuzo zilizotolewa na Zanzibar International Film Festival, anasema kuwa amekuwa na kuwa Lulu mpya mwenye majukumu ya kuelimisha jamii, baada ya kutolewa gerezani kwa dhamana Lulu jambo la kwanza ambalo amelifanya ni kuzindua filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish age.
Filamu ya Foolish age ilizinduliwa Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa filamu, Lulu aliweza kuongea na kuipongeza kampuni inayomsimamia ya Proin Promotion kwa kumpa nafasi ya kuwafunza wengine kwa mambo aliyopitia huku akiwa kama mtoto ambaye hakupenda sana kuwasikiliza wakubwa zake.
Nilitumia fursa hiyo kutaka yeye ni nani aliingiaje katika tasnia ya filamu na kuwa gumzo la filamu anasema kuwa yeye alianza kuigiza akiwa na miaka minne, lakini hakuwa maarufu, lakini akiwa na umri wa miaka saba alikutana na Mahsein Awadh ‘Dr. Cheni’ katika bonaza ambalo pia Dr. Cheni aliaandaa Talent Show, Elizabeth Michael akiwa na mama yake alimweleza Dr. Cheni kama anaweza kuigiza.
“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Bonaza pale Dar west Park ndipo nilipokutana Elizabeth akiwa na mama yake lakini alionyesha maajabu pamoja na udogo aliokuwa nao, katika Talent show yeye aliibuka namba moja huku akiwa amewatupa wasanii wengine mbali hadi Masanja Mkandamizaji alipitwa na Lulu naye akaangukia mshindi wa tatu kwa wakati ule,”anasema Dr. Cheni.
.
Mahsein Awadh
Dr. Cheni akiongea kwa hisia kuhusu msanii wa kike Lulu katika mahojiano.

Dr. Cheni anasema kuwa yeye alimchukua hadi Magomeni na kumkabidhi katika uongoza wa kundi la Kaole Sanaa Group, Lulu alifanyiwa usaili na kupitia kwa asilimiakubwa na kupendwa na kila msanii, lakini jukumu kuu kuhusu usalama na kila jambo lilikuwa kwa Dr. Cheni ambaye baadaye kufuatia mabadiliko ya Lulu kwake Dr. Cheni ilikuwa tatizo kwani kila kitu kibaya kilichofanywa na Lulu lawama ilikuwa kwake kutoka kwa mama yake.
Baada Lulu kuwa mwanakundi la Kaole alichagua jina lake la Nemu na kukubalika na kundi la Kaole na kuanza kuigiza akiwa na kundi hilo na alikuwa ni kipenzi cha waigizaji wote kwani moja ya sifa yake ilikuwa ni usafi na kujipenda toka akiwa mdogo , jambo ambalo hata Herieth Samson ‘Kemmy’ alishikwa na mshangao baada kufungua handbag ya lulu.
.
Herieth Samson kakulu
Kemmy mtu aliyemlea Lulu kisanaa

Mshangao aliopata Kemmy ni pale alipoona vitu ambavyo mara nyingi utakiwa kuwanavyo akina dada lakini Lulu alikuwa na vitu vya kujiremba na kama mtu mzima na hata pale alivyomuuliza vitu vile ni vya nani ? Lulu alimjibu kwa kujiamini tu bila hofu kama ni vitu vyake kwa ajili ya matumizi yake kama mwanamke Kemmy alizidi kushangaa.
“Siku hiyo nilichukua mkoba wa Lulu na kukuta kuna lipstick, poda, leso nyeupe, wanja na kioo, pamoja na funguo wa mlango nikamuuliza vitu hivyo ni vya nani akasema kuwa vyangu mama bwana si unajua kuwa mimi ni msichana kumbuka alikuwa na miaka saba tu, kwa hiyo hayo yalikuwa maisha ya Lulu mtu wa kujipenda,”anasema Kemmy.
Kemmy anasema kuwa baadaye Lulu alizidi kubadilika na kupenda mavazi mafupi ndipo alipomtafauta na kumuomba aongee naye lakini siku hiyo yenyewe alikuwa kava nguo fupi sanaa maana aliamua kumtafuta baada ya kuona picha mbaya katika moja ya gazeti hata hivyo aliongea naye lakini maongezi yale hayakuzaa matunda pale alipopata matatizo na kwenda jela.
Lakini Kemmy anasema Lulu kakua ameonyesha uwepo wa Mungu kwake, Lakini unajua jina la Lulu aliyelitunga na kuwa maarufu? Jina hilo lilitungwa na Salum Mchoma ‘Chiki’ mtunzi wa mchezo wa Tetemo ndiyo alimbadilisha kutoka jina lake la Nemu na kumwita Lulu na leo kweli jina linamaananisha ndoto za Chiki.
“Ndoto zangu zimeonekana wakati ninaandika mchezo wa Tetemo nikampa jina la Dhahabu lakini kwa sababu tulikuwa na uhusiano na Mr. Chuzi akaniomba nibadilishe jina la Dhahabu ili tusiwachanganye watu maana naye alikuwa na Jumba la Dhahabu, ndipo nikampa jina la Lulu hadi leo kawa msanii nyota na Lulu kweli ndoto zangu zimetimia,”anasema Chiki.
Lulu anasema amepitia mengi katika maisha yake hata mama yake anajua mateso aliyompa mambo ambayo hataki kuyarudi kwani kufuatia mkasa ulimpata ilikuwa ni njia moja ya yeye kupata fursa ya kuifundisha jamii kupitia sanaa hiyo na ndiyo maana ameandaa filamu inayoelezea maisha yake akiwa chini ya miaka 18, anatumia kuwaambia vijana wanavyokuwa katika umri huo wasipuuze ushauri kutoka kwa wakubwa zao.
.
Salum Mchoma
Chiki Mchoma aliyempa jina la Lulu.

Elizabeth Michael, mama yake.
Lulu akifurahia na mama yake mzazi katika muziki

Elizabeth Michael.
Lulu akiwa na mama katika pozi.

“Sikumsikiliza mama yangu wakubwa zangu, nilikuwa kizani yale niliyoyafanya ndio niliamini kuwa sahihi, sikuona hatari mbele yangu lakini nahisi ulikuwa mpango wa Mungu kwa tukio lilonitokea, watu walinihukumu lakini ukweli wa hili ni Mungu pekee anayejua ukweli, kwa sasa nampenda Yesu ninaomba na kusali Lulu amekua Lulu ni mpya ninataka kuelimisha jamii kwa kupitia maisha yangu,”anasema Lulu.
Akiongea zaidi alisema kuwa hawezi kuongelea sana mambo yalimtokea kuhusu marehemu Kanumba kwa sababu kesi hiyo bado ipo mahakamani, amepania kufanya kazi kwa nguvu lakini kupitia matatizo yake kajifunza mengi na hataki kurudi huko na anashukru kupata kampuni ya Proin Promotion ambayo ndio wanaomsimamia hawezi kushiriki filamu yoyote kutoka nje ya kampuni hiyo.
.
Elizabeth Michael.
Lulu katika gauni kali na la kuvutia katika pozi.

“Lulu alinitesa hadi nilikuwa napata shida na kuhahaa, lakini nimejifunza kwake kwani mwanangu kabadilika na kuwa mtu mzima anayejua nini anafanya kumbe ilikuwa utoto tu, lakini nimejifunza kutoka kwake mimi nilikuwa mkali sana hiyo ilichangia Lulu kuniogopa na kuwa mbali na mimi pale anapokosa, wazazi tuongee na watoto wetu kwa upole,”anena mama yake.
Lulu ndiyo mlezi wa familia yake mama anafaidika na mtoto wake huku Lulu akimsomesha mdogo wake shule ya kimataifa kwa kumlipia ada na gharama zote, mwenye anasema yupo katika taratibu za kuendelea na shule kwani moja ya malengo yake kuwa mwigizaji wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kupitia filamu anaamini anaweza kufanya hilo Mungu amsaidie.
Baada ya filamu ya Foolish age Lulu anatarajia kutoa filamu ya Mapenzi ya Mungu kazi ambayo amemshirikisha mama yake marehemu Kanumba Frola Mtegoa filamu ambayo nayo bado itakuwa ikiongelea sana maisha na mikasa ya maisha na Lulu ameahidi kutotengeneza wala kuigiza filamu za mapenzi ambazo zimeshamiri Bongo, michezo iliyomtoa Lulu ni, Tetemo, Jahazi, Dira, Tufani,
Gharika na Baragumu.

ASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMUUA MKEWE - KAWE DAR ES SALAM

Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake
Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwa uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia leo.
“Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.
Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.

“Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.

Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anaetafutwa na polisi.
Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

TANZANI YAFUNGWA 2 - 0 NA GAMBIA

20130602-182352.jpgTaifa Stars imemaliza vibaya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika baada ya kufungwa na Gambia huku Kocha Kim Poulsen akisema timu yake imefungwa mabao mepesi.

Wenyeji Gambia wameshinda mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyochezwa leo (Septemba 7 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Independence ulioko hapa jijini Banjul ukiwa ni ushindi wake wa kwanza katika kundi hilo la C ambapo imemaliza ikiwa ya mwisho ikiwa na pointi nne.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Poulsen amesema Gambia ilistahili kushinda kwa vile ilitengeneza nafasi nyingi kuliko timu yake, na kuongeza kuwa mabao iliyopata Gambia yalikuwa mepesi.

“Hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini tukaruhusu mabao mapesi. Nawapongeza Gambia kwani walistahili ushindi. Unapofanya makosa unaadhibiwa. Gambia ilikuwa timu nzuri leo, kwani ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga, sisi tukatoa mabao mepesi,” amesema Kim.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imemaliza katika nafasi ya tatu katika kundi hilo lililokuwa na timu nne ikiwa na pointi sita ilizozipata nyumbani kwa kuzifunga Morocco na Gambia.

Hata hivyo, Kim amesema sababu nyingine ya kutofanya vizuri ni kuwakosa wachezaji wanaocheza nje ya nchi na wengine wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi.

Mabao yote ya Gambia katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Munyemana Hudu kutoka Rwanda yalifungwa na nahodha wa timu hiyo Mustapha Jarjue. Alifunga la kwanza dakika ya 44 na kupachika lingine dakika ya 51, mabao yaliyotokana na wachezaji wa Stars kutokuwa makini.

Katika mechi hiyo Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni/David Luhende, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha/Juma Liuzio.

Taifa Stars inaondoka Banjul kesho (Septemba 8 mwaka huu) saa 6 mchana kwa ndege ya Arik hadi Dakar, Senegal ambapo itaunganisha kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) keshokutwa (Septemba 9 mwaka huu) saa 8.05 mchana.

KIKOSI CHA TANZANIA KILICHOPO DRC NI CHA KULINDA AMANI NA SI KUPIGANA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ) limeeleza kuwa Tanzania haikupeleka kikosi cha jeshi hilo kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)(Monusco) kwa ajili ya kupigana na Rwanda, bali kusaidia kulinda amani.
 
Ufafanuzi huo umekuja siku mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda, kufuatia baadhi vyombo vya habari vikiandika habari jinsi JWTZ kilivyopambana na waasi wa Kikosi cha M23 na kukisambaratisha, sambamba na malumbano kati ya Tanzania na Rwanda.
Askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini wako DRC kwa kazi ya kulinda amani. Malawi bado haijapeleka majeshi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, msemaji wa JWTZ, Meja Erick Komba alisema,“Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya Kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kilichotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (Monusco) na kinafanya kazi chini ya komandi ya Monusco.”
Alifafanua kuwa kazi ya kikosi hicho ni kuzuia waasi kujitanua, kuvunja nguvu yao pamoja na kuwapokonya silaha, huku akisisitiza kuwa sio kweli kuwa Tanzania ilikuwa ikipigana na Rwanda au waasi wa M23, kama ambavyo imekuwa ikielezwa.
“Ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni mwanachama wa nchi za maziwa makuu. Aidha Rwanda imesaidia kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha watu,vifaa na zana nchini kupitia nchi hiyo kwenda DRC,” alisema.
Alisema kuwa vikosi hivyo ambavyo mbali na Waasi wa M23 pia vimekuwa vikipambana na vikosi vya Waasi vya ADF na FDLR, kwamba bado vinaendelea kulinda amani nchini DRC na kama kunaibuka mapambano navyo hulazimika kujibu mapigo.
Kikosi cha Munusco kilianza kupambana na waasi, Agosti 27, mwaka huu na askari wa JWTZ, Khatibu Mshindo alikuwa miongoni mwa waliouawa kwa kupigwa bomu na M23 Mjini Goma ulioko Mashariki mwa DRC. baada ya kuzuka mapigano makali.

BABA KANUMBA ATOA OFA YA KUZAA NA VIBINTI

Charles Kanumba
Baba wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Charles Kanumba ametoa ofa kwa wanawake wanaohitaji kuzaa watoto kama marehemu mwanaye wamuone ili awape uzao wake.
Akipiga stori na paparazi wetu, baba Kanumba alisema amefikia hatua hiyo kutokana na usumbufu anaoupata kwani tangu Kanumba alipofariki dunia wamejitokeza mabinti watano wakidai kuwa ni watoto wake wakati si kweli bali wanahitaji uzao wake.
“Nimechoka kila kona wanatoka vijana na kusema mimi ni baba yao tangu Kanumba alivyofariki dunia. Kama kuna mwanamke anayehitaji uzao wangu, namkaribisha aje nimpe na watoto atakaowazaa watakuwa maarufu sana,” alijigamba baba Kanumba.

KOCHA WA YANGA ADANGANYIKA

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts wakati anaondoka kwenda likizo Ulaya aliacha maagizo kwa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo kumsajili beki Salvatory Ntebe wa Mtibwa. Hata hivyo, badala yake, Kamati ya Usajili ikamsajili Rajabu Zahir kutoka Mtibwa.

Mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa Yanga aliidokeza Mwanaspoti wiki hii kwamba: “Unajua kocha wakati anaondoka kwenda likizo baada ya ligi kumalizika alitaka Kamati ya Usajili imsajili beki wa Mtibwa Sugar yule mrefu mwenye rasta (akimaanisha Salvatory Ntebe) na si huyu wa sasa Zahir (Rajabu).”
Kiongozi huyo alisema Rajabu Zahir amesajiliwa kimakosa kwani chaguo sahihi la Brandts lilikuwa ni yule beki wa kati wa Mtibwa, Salvatory Ntebe mwenye rasta aliyewafunga Simba.
“Ndiye aliyemvutia kocha kwenye mechi ya ligi dhidi ya Simba iliyofanyika Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Mtibwa walishinda 1-0, bao hilo pekee likifungwa na Ntebe.”
Alisema kuwa tangu hapo, Brandts alianza kumsifia beki huyo na kutaka huduma yake kabla ya kupendekeza kamati ya usajili kumsajili ili asaidiane na Kelvin Yondan ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’
Hata hivyo, alieleza kuwa Brandts aliporejea na kukutana na kamati hiyo aliambiwa Mtibwa waligoma kumtoa na kutaja gharama kubwa, ndipo walipoamua kumsajili Zahir.
Brandts alipoulizwa na Mwanaspoti kuhusu hilo alishangaa mwandishi amejuaje? Lakini akagoma kutolea ufafanuzi kwa madai si wakati wake na hakuna kiongozi yeyote wa kamati ya usajili aliyetaka kupokea simu kutamka lolote.
Hata hivyo, Brandts amesoma uwezo wa Zahir na kumwingiza kwenye programu yake huku akimsifia kama mchezaji mdogo anayependa kujifunza na kujituma zaidi.
Zahir ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri msimu uliopita lakini Ntebe anamzidi kwa kitu kimoja tu. Uzoefu na utulivu uwanjani

KISA CHA MWANAMKE ANAYEDAI AMEZAA NA DIAMOND

Mrembo aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.

Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.

Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.

Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.

Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.

Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.

Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.

Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.

Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.

Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.

‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.

Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.

Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.

Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya  na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.

Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.

Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. 

Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.

Baada ya kupata madai hayo, gazeti hili lilimsaka Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena,  naye aliacha kumfuatilia.

“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.

PICHA ZA WASANII MBALIMBALI (WEMA, KAJALA, DULLY, TID NA WENGINE WASHANGWEKA KIOTA CHA THAI VILLAGE

IMG_4546
Pichani juu na chini ni Wema Sepetu akimpagawisha Sam Mapenzi wa Skylight Band
IMG_4552
Sam Mapenzi akimwimbia Wema Sepetu ndani kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar Juma lililopita.

IMG_4374
Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lucos akitoa burudani huku akisindikizwa na mwimbaji mwenzake Digna.
IMG_4421
Superstar Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa na mrembo wa kizungu pamoja na JEMBE wakishow love mbele ya camera yetu.
IMG_4412
Maimatha wa Jesse akishow love na marafiki alipotinga kwenye kiota cha Thai Village kuanza week end yake na burudani za Skylight Band.
IMG_4370
Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
.
IMG_4433
Sam Mapenzi akicheza sambamba na mashabiki wa Skylight Band..... palikuwa hapatoshi.
IMG_4456
Wema Sepetu akiwasili kiota cha Thai Village na kuwasabahi vijana wa Skylight Band kuonyesha kuwakubali kwa burudani yao.
IMG_4460
Furaha na tabasamu bashasha vilitawala usoni kwa mwanadada Wema Sepetu.
 
IMG_4484
Kila mtu alijinafasi kwa style ya aina yake.....wenye kupinda mgongo haya kwa raha zao.
IMG_4494
Wema Sepetu akifurahi jambo na mashabiki wake ndani ya kiota cha Thai Village kilichopo Masaki jijini Dar.
IMG_4498
Mduara ulihusika kama kawaida.
IMG_4507
Wema Sepetu na Kajala wakibadilishana mawazo huku burudani ya Skylight Band ikiendelea.
IMG_4555
Petit Man naye hakukubali kulishindwa akamuonyesha Wema ufundi wake kwa kusakata Sebene la Skylight Band.
IMG_4473
Ukumbi ulilipuka ni nomaaa kama inavyoonekana pichani.
IMG_4477
Wadau wa Skylight Band bila kukosa wakiwakilisha Kijitonyama.
Wadau wa ukweli wenye mapenzi na Skylight Band camera yetu uliwamulika.
IMG_4482
Wasanii wa Bongo Flava kutoka kushoto ni Shetta, TID pamoja na Dully Sykes nao walikuja kula bata na Band ya vijana, wakubwa kwa watoto yenywe Swaggaz za ukweeeh Skylight Band.

MEMBE AMEZITAKA NCHI ZA KENYA, UGANDA NA RWANDA KUELEZEA KILE WALICHOKIJADILI BILA YA KUISHIRIKISHA TANZANIA

Serikali imeziomba nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuipa taarifa ya mikutano waliyoifanya bila ya kuishirikisha hivi karibuni. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumzia na waandishi wa habari ofisini kwake jana alisema wameziomba nchi hizo kuitaarifu kile walichokijadili.
Alisema kwakuwa nchi hizo ni miongoni mwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zilitakiwa kutoa maelezo kwa Umoja huo ili kila nchi wanachama ziweze kutambua lengo lao.
Membe alisema pia Serikali ya Tanzania, imeziomba nchi hizo kuwapa maelezo ya kile walichokuwa wakikijadili katika mkutano wao wa hivi karibuni uliofanyika Kenya.
“Tumewaomba wenzetu hawa, kutueleza mkutano wao ulikuwa unahusu nini, kwani tulipaswa kujua kutokana na kuwa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata kama hawakutaka kutushirikisha,” alisema Membe na kuongeza: “Nawaomba Watanzania wenzangu wasiwe na wasiwasi juu ya mkutano huo, kwani tuna kila kitu hapa nchini. Hatuna haja ya kuanza kufikiri mambo ambayo hayana msingi wowote.”
Alisema uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeanza kuimarika baada ya marais wa nchi hizo, Jakaya Kikwete na Paul Kagame, kukubaliana kuanza mazungumzo yatakayokuwa yakifanyika katika nchi hizo.
Membe alisema Rais Kikwete na Rais Kagame, walikutana peke yao, wakiwa na lengo la kuelezana na kuelimishana mambo mbalimbali na walikubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
“Rais Kikwete amesema mkutano ulikuwa mzuri, wamezungumza mambo mengi na wamekubaliana kuanza kufanya mazungumzo yatakayokuwa yakifanyika Tanzania na Rwanda, hii itakuwa ni kuimarisha uhusiano wetu na wao,” alisema Membe.
“Hali hii inakata majungu, uongo na fitna zilizokuwa zikienezwa na watu, ambavyo vingeweza kusababisha kutokuelewana baina yetu na wenzetu wa Rwanda.”
Alisema katika mkutano huo, marais hao walielezana, kuchambua na kujadili ukweli, lengo likiwa ni kurudisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

JE, WAZIFAHAMU SABABU ZA MALUMBANO SIKU YA JUMATANO NA ALHAMISI BUNGENI - DODOMA

Maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa 2013 yanadaiwa kuwa yalibadilishwa dakika za mwisho na kwamba suala hilo ndicho kiini cha vurugu zilizotokea bungeni mjini Dodoma juzi.

Gazeti la Mwananchi limefanikiwa kuona nakala inayodaiwa kuwa ni maoni ya awali ya kamati hiyo ambayo yalikuwa na mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa marekebisho kadhaa kwenye muswada huo, tofauti na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na Mwenyekiti wa Kamati, Pindi Chana.
Jumatano na Alhamisi wiki hii kulikuwa na mvutano mkubwa bungeni kiasi cha wabunge wa upinzani kutoka vyama vitatu vya NCCR -Mageuzi, Chadema na CUF kuungana na kususia mjadala kuhusu muswada huo.
Imedokezwa kuwa mvutano mkali kuhusu muswada huo ulianza ndani ya kamati hiyo wakati wajumbe wake ambao ni wabunge wa CCM walipotumia wingi wao kubadili maoni ya awali na kuweka maoni mapya, hatua ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa na msukumo wa Serikali nyuma yake.
Ndani ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, wabunge wa upinzani ambao kwa idadi yao ni wachache walishindwa kuzuia mabadiliko hayo ya “lala salama” yanayodaiwa kuwa yaliwekwa Septemba 2, mwaka huu, hivyo waliazimia kuhamasisha wabunge wote wa upinzani kupinga marekebisho hayo kutokana na sababu kuu mbili.
Sababu hizo ni kutofanyika kwa mikutano ya wazi kwa umma (public hearing) upande wa Zanzibar na hatua ya kuwapo kwa mapendekezo ya Rais kurundikiwa madaraka makubwa ya uteuzi wa wabunge kutoka asasi za kijamii watakaoingia katika Bunge la Katiba.
Habari zinasema wakati fulani Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alitembelea kamati hiyo wakati ikiedelea na vikao vyake na kukuta mvutano mkali kuhusu suala la marekebisho ya sheria ya sheria hiyo na alishauri kwamba pale ambapo hawataweza kuelewana basi wasubiri uamuzi ndani ya Bunge.
Jana gazeti hili lilimtafuta Chana kupitia simu yake ya mkononi na baada ya kumweleza kuhusu madai hayo alisema: “Tafadhali sana kwa sasa niko kwenye kikao, kwanza simu yako nimeipokea kwa heshima tu, tutafutane wakati mwingine”.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alikiri kwamba kulikuwa na mapendekezo ya kuongeza idadi ya wabunge na namna ya kuwapata, lakini Serikali iliyakataa katika hatua ya majadiliano kabla ya suala hilo kufikishwa bungeni.
Tofauti ya maoni
Nakala ya taarifa ya awali ilipendekezwa kuwa katika kuteua wajumbe 166 wa Bunge la Katiba, Rais azingatie kikamilifu mtiririko wa mapendekezo ya kila kundi lililoainishwa katika kifungu cha (1) (c).
“Na endapo Rais hatazingatia mapendekezo ya kundi mojawapo, Rais afanye mrejesho kwa taarifa kwa kundi husika juu ya sababu za kutozingatia mtiririko wa mapendekezo yaliyowasilishwa kwake,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa kamati hiyo ilikuwa na maoni kwamba makundi mengine ya kijamii yaongezwe katika kifungu cha 22(1) (c) cha sheria mama, ili kupanua wigo wa uwakilishi mpana katika Bunge la Katiba, hivyo kuongeza idadi ya wabunge hao kutoka idadi ya awali 166 hadi kufikia 201.
“Kamati inashauri kuwa idadi ya wajumbe iwe 201 badala ya idadi ya wajumbe 166 iliyotajwa katika sheria mama, ili kupata idadi ya wajumbe watakaounda Bunge Maalumu la Katiba,” inasomeka taarifa hiyo.
Hata hivyo, maoni hayo yanatofautiana na yale yaliyowasilishwa bungeni juzi na jana, kwani yanaonyesha kwamba kulikuwa na majadiliano na mashauriano baina ya kamati na Serikali, hivyo ilikubaliana kuwa “Rais apewe mamlaka ya kufanya uteuzi wa wajumbe Bunge la Katiba” huku idadi ya wabunge wa kuteuliwa wakibaki 166.
Kifungu hicho kiliondoa haki ya kila taasisi kuteua jina la mjumbe wake katika Bunge hilo na badala yake, ikapendekezwa kuwa Rais atapelekewa matatu ili ateue moja kati ya hayo.
Hata hivyo, jana wakati Bunge lilipoketi kama kamati kwa ajili ya kupitia vifungu vya marekebisho ya muswada huo, Serikali iliwasilisha marekebisho ya nyongeza ambayo yanazitaka asasi za kiraia ziteue majina tisa na kati ya hayo Rais anaweza kuteua jina moja na kama asiporidhika anaweza kuteua mtu kutoka nje ya orodha hiyo.
Kuhusu suala hilo Chikawe alisema: “Tangu awali ilikuwa inaonyesha wajumbe ni 166. Ni kweli Kamati ilipendekeza wajumbe hao waongezeke hadi 201 lakini pendekezo hilo halikukubaliwa, ikabakia wajumbe watakuwa 166.”
Ushiriki wa Zanzibar
Itakumbukwa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilipewa wiki nne za kuendesha vikao vyake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Bunge uliomalizika jana, tofauti na kamati nyingine ambazo zilipewa wiki mbili.
Baadhi ya wabunge (hasa wa upinzani) wanasema madhumuni ya kupewa muda huo ni kama hayakutimia kwani hawakuweza kupokea maoni kutoka kwa makundi muhimu hasa ya upande wa Zanzibar kama ilivyokusudiwa.
Hata hivyo, jana Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Balozi Seif Ali Idd, alilihakikishia Bunge kuwa upande wa Zanzibar ulishirikishwa katika kutoa maoni ya muswada huo.
Hatua ya Balozi Idd kutoa ufafanuzi ilitokana na mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba(CCM) aliyeomba kwa vile Balozi Seif yuko ndani ya Bunge basi apewe fursa kufafanua utata huo.
Kauli ya Balozi Idd inapingana na ile iliyotolewa juzi jioni na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye alisema ni kosa kubwa kamati kutochukua maoni ya Wazanzibar.

Lissu alisema kulikuwa na njama tangu mwanzo za kuhakikisha kuwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala haichukui maoni ya Wazanzibari na hilo linathibitishwa na ratiba zilizokuwa zimeandaliwa na kamati.
“Katika orodha ya wadau wote 22 waliokuwa wameorodheshwa katika kutoa maoni yao juu ya muswada huu hakukuwa na Mzanzibari hata mmoja…tulipoipitia tukasema hapana Wazanzibari wako wapi,” alisema.
Lissu alisema yeye, Mwenyekiti wa Kamati, Chana na Makamu Mwenyekiti, William Ngeleja walikwenda kumwona Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na kumweleza azma yao ya kwenda kuzungumza na wadau wa Zanzibar.
“Katibu akatwambia kwamba yeye ana fedha za kutuwezesha kukaa Zanzibar hata wiki moja, kwa hiyo tukarudi kwenye kamati tukatengeneza ratiba mpya na tukaongeza wadau sita wa Tanganyika na Wazanzibari wanane,” alisema Lissu.
Aliwataja wadau hao kuwa ni Chuo cha Taifa Zanzibar, Chuo Kikuu cha Zanzibar, Chama cha Mawakili Zanzibar, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar, Chama cha Walemavu Zanzibar na Profesa Abdul Shariff.
Wadau wengine walikuwa ni Shirikisho la Vyama visivyo vya Kiserikali Zanzibar (Angoza) na Jumuiya ya Misikiti Zanzibar na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, lakini hatukuwahi kukutana nao na kupokea maoni yao.
“Tukakubaliana kuwa tutakaa Zanzibar kwa siku tatu kuanzia Julai 14 hadi Julai 16 mpaka leo hatujawahi kuambiwa kwa nini tulizuiwa kwenda Zanzibar, lakini maneno yaliyokuwa yakisikika eti kwa sababu za kiusalama,” alisema.
Lissu alisema wakati kamati yao ikiambiwa haiwezi kwenda Zanzibar kwa sababu za kiusalama, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge hilo ilikuwa Pemba ikiendelea na ziara zake.