Friday, February 15, 2013

MSANII MAARUFU WA NIGERIA (GOLDIE HARVEY) AMEFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa kinigeria na aliyekua mshiriki wa Big Brother Africa House of Talent Goldie Harvey amefariki Dunia.

Goldie Harvey
Msanii huyu alizaliwa Susan Filani, na amefariki alhamisi usiku, katika hospitali ya Roddington iliyopo katika kisiwa cha Victoria-Lagos Nigeria.

RAIS KIKWETE, MWINYI NA MKAPA WASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU LAIZER


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakishiriki ibada ya Mazishi ya Askofu Dkt.Thomas Laizer iliyofanyika katika kanisa na Usharika wa mjini Kati.mjini Arusha leo.

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati,Arusha mjini leo.

Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe wakati wa Mazishi ya Skofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati
 (picha Zote na Freddy Maro)

NSSF YAANDAA MPANGO WA KUONDOA UMASKINI

Mfuko wa hifadhi ya jamii hapa nchini(NSSF)umesema kuwa kwa sasa unaandaa mpango maalumu ambao utalenga kuondokana na Umaskini wa Nchi ya Tanzania huku mpango huo pia ukiongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile Ajira na Vipato vya wananchi

Hayo yameelezwa  leo mjini Arusha na Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Dkt Ramadhani Dau   wakati akiongea na wadau wa mfuko katika mkutano wa tatu unaoendea mjini Arusha.

SAYARI MPYA (2012 DA 14) KUPITA KARIBU NA DUNIA LEO USIKU

Usiku wa leo, sayari ndogo itaikosakosa dunia kwa umbali wa kilomita 27,000

Sayari hiyo iliyopewa jina la 2012 DA 14 ina kipenyo cha mita 68, na uzito wa tani laki nne itapita karibu na dunia saa nne na dakika ishirini na tano kwa saa za Afrika Mashariki, hii ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la anga la Ulaya, ESA.  

Thursday, February 14, 2013

MISA TAKATIFU YA MAZIKO YA ASKOFU AMEDEUS MSARIKIE MOSHI


Misa Takatifu ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi Amedeus Msarikie inaendelea katika Kanisa la Kristo Mfalme Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Misa ya Leo inaongozwa na Baba Askofu Tarsisius Ngalalekumtwa ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Tanzania. 

Monday, February 11, 2013

BREAKING NEWS

Habari zilizopo ni kuwa leo Geita mapigano yametokea kati ya Waislamu na Wakristo (particular Protestants wa AIC). Na hii ni baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo wao,maeneo ya Katoro na jirani ni vurugu na mtifuano!

ASKOFU MSARIKIE KUZIKWA FEB 14 MOSHI


Askofu Mstaafu  Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki Moshi, aliyefariki dunia hivi karibuni, anatarajiwa kuzikwa kwenye Kanisa kuu la Kristu Mfalme, Jimbo Katoliki Moshi, hapo tarehe 14 Februari 2013.

Sunday, February 10, 2013

NECTA-MATOKEO YA KIDATO CHA NNE BADO


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpTl85E_9puVvP_hTe-LHgQNY_Vf7jHqZs4tpSBAC5azL1j9Cfk2erlatq9G9lOjUzzb3r4_Pw-DPG6niaTnAvKKvc2CCvHW2BBuGULYMkdiJ6Df78JEeIuSuOPWdQY8Kv7IWHaATjGH4/s1600/exam-results+%25281%2529.jpg

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema  matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.

Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa  ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari.

Akizungumza na mwandishi jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi alisema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).

Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.

Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.