Serikali ya Bulgaria imejiuzulu kufuatia kufanyika maandamano ya nchi nzima kupinga hatua za kubana matumizi na kupanda kwa gharama za umeme.
Waziri Mkuu wa Bulgaria Boiko Borisov ametangaza taarifa hiyo hivi leo na kuliambia bunge la nchi hiyo kuwa hawezi kuendelea kuwa ndani ya serikali ambayo jeshi la polisi linawapiga wananchi. Borisov amesema kuwa wao kama viongozi wana utu na heshima na wanatambua kuwa ni wananchi ambao wameiweka serikali madarakani lakini anashangaa kuona hivi leo serikali inawanyanyasa raia hao. Bulgraia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya ambayo ina umasikini mkubwa. Imekumbwa na wimbi la maandamano la wananchi wanaolalamikia hali ngumu ya maisha.
No comments:
Post a Comment