Sunday, September 8, 2013

T.D JAKES AOMBEWA NA MUIGIZAJI TYLER PERRY

Vipi siku Masanja Mkandamizaji anamuwekea mkono Mwalimu Christopher Mwakasege na kumuombea, hakika wengi watashangaa na kudhani labda ni utani. Lakini la hasha, Mungu hutumia chombo chochote, hivi ndivyo ilivyokuwa Potter's House, kwenye huduma ya T.D Jakes, ambapo muandaaji (producer) na msanii muigizaji maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla, Tyler Perry - alipomuwekea mkono Askofu T.D Jakes.

Tukio hilo limetokea mwanzoni wa wiki iliyopita ambapo hudu aya vijana likuwa inaanzishwa kanisani hapo, na ndipo Tyler alipokaribishwa kutoa mchango wake. Hapo awali Tyler alifikiria kutoa dola laki moja kumi na tatu elfu, lakini alipopanda jukwaani, Mungu alizungumza nae kwa namna nyingine, na ndipo alipoamua kutoa dola milioni moja, sawa na takriban bilioni moja za Kitanzania.


Gospel Kitaa imeshuhudia video hiyo ambapo wakati Tyler akieleza kuhusu kutii sauti ya Mungu na umuhimu wa kutoa, ndipo muandaaji huyo alipoonekana dhahiri kujizuia ili asihubiri, na kutaka kukabidhi kipaza sauti, lakini uzuri ni kwamba hakikupokelewa kama alivyotarajia. Baada ya hapo Tyler Perry akaanza kumnenea maneno ya baraka Askofu Jakes, ambaye naye bila hiyana alikuwa tayari kupokea baraka za Mungu, ambapo alimsogelea Perry na kunyoosha mikono yake kama ishara ya utii, na hapo ndipo Roho Mtakatifu alipochukua nafasi yake, na kisha Tyler Perry kumuwekea mkono Askofu Jakes, ambapo wasaidizi waliwahi ili kumshikilia kwa nyuma.

Kati ya vitu ambavyo Tyler Perry alihubiri kwa dakika chache sana, ni kwamba usitumie muda mwingi kutafakari kuhusu wanachokuwazia maadui zako, bali kumbuka kuwa ili ubarikiwe, basi hao wabaya wako watakuwepo, ndio maana Biblia inasema atakuandalia meza mbele yao. Tazama video na ushuhudie mwenyewe kilichojiri kwa utukufu wa Mungu.

Muigizaji, Tyler Perry akimnenea baraka Askofu T.D Jakes wa the Potter's House

No comments:

Post a Comment