Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake |
Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa
jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya
kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta
Mkali.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za
mauaji hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa
Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo
akisema kwa uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa
kuamkia leo.
“Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na
inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa
uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,”
alisema.
Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua
Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka
asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye
huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa
na majeraha pamoja na damu.
“Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani
kwa mama kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha
kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini.
Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta
amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na
machozi.
Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anaetafutwa na polisi.
Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. |
Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. |
No comments:
Post a Comment