Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela amelazwa hospitalini kwa kile kinachoelezwa kwamba ukaguzi wa afya yake ambao ulikuwa umepangwa kabla.
Kulazwa kwake kunakuja miezi kadhaa kufuatia kulazwa hospitali kwa mara ya mwisho kwa Mzee Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambapo alipatiwa matibabu kutokana na maambukizi ya mapafu pamoja na kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa vijiwe kwenye nyongo.
Alikaa hospitalini kwa siku 18 ambao ulikuwa muda mrefu kubakia hospitalini tokea kuachiwa kwake kutoka gerezani hapo mwaka 1990. Mandela ametumikia kipindi kimoja akiwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini baada ya kushinda uchaguzi hapo mwaka 1994.
Hali ya Mandela ambaye ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel hapo mwaka 1993 pamoja na Rais wa mwisho wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini FW De Clerk imekuwa ikizidi kudhoofika katika miaka ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment