Wagombea urais nchini Kenya, usiku huu wanashiriki katika mdahalo wa pili na wa mwisho, ikiwa ni wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Machi 4.
Mgombea urais wa muungano wa Jubilee, Uhuru Muigai Kenyatta, aliashiria awali kuwa hatashiriki kwenye mdahalo huo, lakini sasa yupo katika mdahalo huo. Mdahalo huo utazingatia zaidi masuala ya ardhi na maendeleo ya kiuchumi. Mdahalo wa unahudhuriwa na kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya, rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano na rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae. Mdahalo wa kwanza ulifanyika tarehe 11 ya mwezi huu wa Februari, ambapo uligusia masuala ya ukabila, rushwa, usalama, elimu na huduma ya afya. Katika mdahalo wa kwanza, wagombea wote wanane wanaowania kiti cha urais walishiriki.
No comments:
Post a Comment