Amri ya rais iliyosomwa kupitia televisheni ya taifa, ilifuta amri nyingine ya Aprili 22, 2011,inayohusiana na uteuzi wa serikali. Chini ya makubaliano ya amani, serikali mpya itaongozwa na mjumbe wa kisiasa kutoka upinzani, na kuandaa uchaguzi wa wabunge ndani ya miezi 12 kuchukua nafasi ya bunge la sasa linalodhibitiwa na washirika wa Bozize.
Makundi matano yanayounda muungano wa Seleka yalikubali kusitisha mapigano kufuatia makubaliano hayo, na hivyo kukomesha kitisho kikubwa zaidi kwa utawala wa muongo mmoja wa Bozize.
No comments:
Post a Comment